Call forwarding ni kitendo cha kuelekeza simu yako ipokelewe na mtu mwingine au ipokelewe kwenye simu nyingine. Mfano simu yako wataka kuacha ipeleke chaji au hutaki kutembea nayo ,hivyo waweza tumia call forwading kupokea simu zitakazokuwa zinapigwa wakati ukiwa haupo karibu na simu yako. Watu wengi hutumia call forwading kwa malengo mabaya mfano kufatilia maongezi ya mpenzi wake au mtu yeyote yule ambaye anatamani kujua maongezi yake na watu wengine kitu ambacho ni kinyume na sheria.
Machaguo katika call forwarding :-
1.Always forward simu zako zote zitaelekezwa kwenda katika namba nyingine na kupokelewa.
2.Forward when busy simu zako zote zitaelekezwa kwenda katika namba nyingine ikiwa simu yako inatumika (busy)
3.Forward when unreachable simu zako zote zitaelekezwa katika namba nyingine ikiwa namba yako haipatikani
4.Forward when unanswered simu zako zote zitaelekezwa katika namba nyingine ikiwa haujapokea.
zifuatazo ni code za call forwading
*#62# hizi code hutumika kujua kama umeunganishwa na call forwarding na utaona namba ulio unganishwa nayo tofauti na hapo basi utakuwa haujaunganishwa.
*21*Namba ya simu# code hizi zitatumika ku forward simu zako zote na zitaelekezwa kwenda katika namba nyingine utakayoitaka(Always forward)
*61*Namba ya simu # code hizi zitatumika ku forward simu zako zote na zitaelekezwa katika namba nyingine ikiwa haujapokea(Forward when unanswered )
*62*Namba ya simu # Code hizi hutumika ku forward simu zako zote kwenda katika namba nyingine pale tu simu yako itakapokuwa haipatikani yawezekekana simu imezimika au upo sehemu isiyo na mtandao(Forward when unreachable)
*67*Namba ya simu # Code hizi hutumika ku forward simu zako zote kwenda katika namba nyingine pale tu simu yako itakapokuwa simu zako zote zitaelekezwa kwenda katika namba nyingine ikiwa simu yako inatumika (Forward when busy)
Asante kwa kusoma ,endelea kutembelea tovuti hii kwa kupata kujua mambo mengi zaidi.
No comments:
Post a Comment