Jinsi ya kutoa pattern au password kwenye Android Smartphones.
Kwanza; Izime simu yako kisha toa Memory Card pamoja na Sim card(laini yako) ,endapo utaacha kuna hatari ya kupoteza vitu vyako vya msingi vilivyo kwenye Memory card na laini yako.
Pili; Iwashe simu kwa kubonyeza kitufe cha kuongeza sauti pamoja na cha kuwashia simu kwa pamoja na vishikilie mpaka simu itakapowaka kwa kukupeleka kwenye option ya recovery mode.
NB: Hiyo hatua ya pili kwa baadhi ya simu ili upate kufika kwenye recovery mode yakupasa ufanye mambo yafuatayo.
Bonyeza volum up (Ni kitufe cha kuongeza sauti) + home( Ni kitufe cha Nyumban) + power( Ni kitufe cha kuwasha simu)
AU
AU
Baada ya simu kuwaka na kuleta Recovery mode fuata mambo yafuatayo ambayo yatuingiza hatua ya tatu ambayo ni;
Tatu;Hapo Tumia button za sauti kwa kupandisha au kushusha na kuchagua wipe data au factory reset au mstari wa tatu kutoka chini kwa simu zenye maandishi ya kichina kisha bonyeza kitufe cha kuwashia simu ,hicho hutumika kumaanisha OK.Hapo Simu itaanza ku-reset yenyewe.
Nne;chagua Option ya restart.Hapo Simu yako itawaka ikiwa kama ilivyotoka dukani yani itakuwa haina tena passwords wala pattern na vitu vyote ulivyokuwa umehifadhi kwenye simu vitafutika pia.
Asante kwa kusoma , karibu sana na endelea kufatilia JifunzeTech-2021 upate kujifunza na kujua zaidi mambo mbalimbali kuhusu simu,mtandao,computer n.k . Pia usisahau kuandika comment zako hapo chini kwani ni za muhim sana.
asante
ReplyDeleteInaniandikia na no command
ReplyDeleteAsante
ReplyDeleteInaleta fastboot mode
ReplyDelete