Showing posts with label simu. Show all posts
Showing posts with label simu. Show all posts

Saturday, April 17, 2021

Ku forward calls bila kutumia code(Ku forward calls kwa kufanya setting kwenye simu yako)

Zipo aina au machaguo mengi kwenye call forwarding hivyo yaweza kuwa ni vigumu kukalili code zote ili upate kuweza kuzitumia. zifuatazo ni njia ambayo itakusaidia kuweza kufanya call forwarding bila kutumia codes.

Hatua ya kwanza nenda kwenye setting

Hatua ya pili baada ya kubonyeza sehemu ya setting chagua call

Hatua ya tatu baada ya kuchagua call, chagua call forwarding

Hatua ya nne baada ya kuchagua call forwading ,chagua voice call

Hatua ya tano baada ya kuchagua voice call ,chagua aina ya call forwading unayoitaka(always forward ,forward when busy, forward when unanswered,forward when unreachable)

Hatua ya sita andika namba utayo ambayo simu zote zitakazokuwa zinapigwa zitakuwa zinapelekwa huko na kupokelewa huko.

baada ya kuweka hiyo namba utakuwa tayari umefanikiwa kuunganisha call forwarding kikamilifu, na utaona alama kwa juu ya simu yako ikiashiria simu imefanyiwa call forwarding.

Kama utapenda kujua kufanya setting za call forwarding kwa kutumia code ,rejea katika post zangu zilizopita.

Jinsi ya kupata IMEI ( International Mobile Equipment Identity) ya simu yako

Neno IMEI ni kifupi cha International Mobile Equipment Identity. IMEI Ni number ambayo inatumiwa kukitambua na kutofautisha vifaa ambavyo vinatumia cellular network na huwa zipo tarakimu 15 katima IMEI . Cellular network ni network ambayo unatumia kupiga simu au kuunganishwa na internet. Kama simu yako ina sim card (laini) mbili,basi na IMEI zitakuwa mbili.

Umuhimu wa IMEI kwenye simu yako

1.Husaidia kuzuia wizi wa mobile devices.

2.kutambua na kutofautisha mobile devices pale inapoconnect kwenye mnara

Jinsi ya kupata au kujua IMEI ya simu yako.

1.kama simu yako ni ya kutoa betri ,IMEI waweza ipata kwa kuangalia nyuma ya simu yako baada ya kutoa betri la simu yako.

2.kama simu yako hairusu kutoa betri , utaweza kujua IMEI ya simu yako kwa kupiga code zifuatazo * # 06 #.

3. Kwa kwenda kwenye setting ya simu yako

Hatua ya kwanza. Nenda kwenye setting ya simu yako.

Hatua ya pili. Baada ya kubonyeza na kuingia kwenye setting za simu yako , chagua sehemu walipoandika about device

Hatua ya tatu. Baada ya kubonyeza sehemu ya abot devive hatua inayofata bonyeza status.

Hatua ya nne.Baada ya kubonyeza sehem iliyoandikwa status kinachofata ni kuona IMEI namba ya simu yako

NB; Ukifanya update zozote zile kwenye simu yako au ukibadilirisha sim card zako, IMEI number haibadiliki kwasababu imetengenezwa kama sehemu ya hardware ya simu. Wapo watu wanao badilisha IMEI namba na inawezekana lakini ni kosa kisheria kwa baadhi ya nchi.

JINSI YA KUONDOA CALL FORWARDING KATIKA SIMU YAKO

JINSI YA KUONDOA CALL FORWARDING KATIKA SIMU YAKO Kama uli fanya setting za kuforwad simu kwenye simu yako na ukashindwa kutoa au wahisi kuna mtu ameforward simu zako kwenda kwenye namba yake basi code zifuatazo zitakusaidia kuondoa call forwarding zote kwenye simu yako.

##002# hizi code hutumika kuondoa call forwarding zote kwenye simu yako.

Kama wataka kujua maana na jinsi ya kuforward calls ,angalia post zangu zilizopita na huko utapata kujua yote kuhusu call forwarding.

CALL FORWARDING( KU FORWARD SIMU )

CALL FORWARDING( KU FORWARD SIMU )

Call forwarding ni kitendo cha kuelekeza simu yako ipokelewe na mtu mwingine au ipokelewe kwenye simu nyingine. Mfano simu yako wataka kuacha ipeleke chaji au hutaki kutembea nayo ,hivyo waweza tumia call forwading kupokea simu zitakazokuwa zinapigwa wakati ukiwa haupo karibu na simu yako. Watu wengi hutumia call forwading kwa malengo mabaya mfano kufatilia maongezi ya mpenzi wake au mtu yeyote yule ambaye anatamani kujua maongezi yake na watu wengine kitu ambacho ni kinyume na sheria.


Machaguo katika call forwarding :-

1.Always forward simu zako zote zitaelekezwa kwenda katika namba nyingine na kupokelewa.

2.Forward when busy simu zako zote zitaelekezwa kwenda katika namba nyingine ikiwa simu yako inatumika (busy)

3.Forward when unreachable simu zako zote zitaelekezwa katika namba nyingine ikiwa namba yako haipatikani

4.Forward when unanswered simu zako zote zitaelekezwa katika namba nyingine ikiwa haujapokea.

zifuatazo ni code za call forwading

*#62# hizi code hutumika kujua kama umeunganishwa na call forwarding na utaona namba ulio unganishwa nayo tofauti na hapo basi utakuwa haujaunganishwa.

*21*Namba ya simu# code hizi zitatumika ku forward simu zako zote na zitaelekezwa kwenda katika namba nyingine utakayoitaka(Always forward)

*61*Namba ya simu # code hizi zitatumika ku forward simu zako zote na zitaelekezwa katika namba nyingine ikiwa haujapokea(Forward when unanswered )

*62*Namba ya simu # Code hizi hutumika ku forward simu zako zote kwenda katika namba nyingine pale tu simu yako itakapokuwa haipatikani yawezekekana simu imezimika au upo sehemu isiyo na mtandao(Forward when unreachable)

*67*Namba ya simu # Code hizi hutumika ku forward simu zako zote kwenda katika namba nyingine pale tu simu yako itakapokuwa simu zako zote zitaelekezwa kwenda katika namba nyingine ikiwa simu yako inatumika (Forward when busy)



Asante kwa kusoma ,endelea kutembelea tovuti hii kwa kupata kujua mambo mengi zaidi.

Thursday, April 15, 2021

JINSI YA KUTOA PATTERN KWENYE SIMU YAKO WEWE MWENYEWE BILA KUFLASHI KWENYE SIMU

JINSI YA KUTOA PATTERN KWENYE SIMU YAKO WEWE MWENYEWE BILA KUFLASHI KWENYE SIMU Je umesahau pattern yako au password kwenye simu yako ya smartphone na wataka kutoa lock na hauna kompyuta au hauna pesa kulipa ili usaidiwe kutoa pattern au password.
Zifuatazo ni mbinu zitakazo kusaidia kuweza kutoa pattern kwenye simu yako ya mkononi bila ya hata kutumia njia ya kuflashi kwenye kompyuta

Jinsi ya kutoa pattern au password kwenye Android Smartphones.



Kwanza; Izime simu yako kisha toa Memory Card pamoja na Sim card(laini yako) ,endapo utaacha kuna hatari ya kupoteza vitu vyako vya msingi vilivyo kwenye Memory card na laini yako.

Toa Memory Card pamoja na Sim card(laini yako)



Pili; Iwashe simu kwa kubonyeza kitufe cha kuongeza sauti pamoja na cha kuwashia simu kwa pamoja na vishikilie mpaka simu itakapowaka kwa kukupeleka kwenye option ya recovery mode.


NB: Hiyo hatua ya pili kwa baadhi ya simu ili upate kufika kwenye recovery mode yakupasa ufanye mambo yafuatayo.


Bonyeza volum up (Ni kitufe cha kuongeza sauti) + home( Ni kitufe cha Nyumban) + power( Ni kitufe cha kuwasha simu)

AU
Volume down ( Ni kitufe cha kupunguza sauti ) + power ( Ni kitufe cha kuwasha simu)
AU
Volume up (Ni kitufe cha kuongeza sauti) + power( Ni kitufe cha kuwasha simu)

AU
Volume down ( Ni kitufe cha kupunguza sauti )+ home ( Ni kitufe cha Nyumban) + powe r( Ni kitufe cha kuwasha simu)

AU
Home( Ni kitufe cha Nyumban) + power ( Ni kitufe cha kuwasha simu)



Baada ya simu kuwaka na kuleta Recovery mode fuata mambo yafuatayo ambayo yatuingiza hatua ya tatu ambayo ni;

Tatu;Hapo Tumia button za sauti kwa kupandisha au kushusha na kuchagua wipe data au factory reset au mstari wa tatu kutoka chini kwa simu zenye maandishi ya kichina kisha bonyeza kitufe cha kuwashia simu ,hicho hutumika kumaanisha OK.Hapo Simu itaanza ku-reset yenyewe.

Nne;chagua Option ya restart.Hapo Simu yako itawaka ikiwa kama ilivyotoka dukani yani itakuwa haina tena passwords wala pattern na vitu vyote ulivyokuwa umehifadhi kwenye simu vitafutika pia.





Asante kwa kusoma , karibu sana na endelea kufatilia JifunzeTech-2021 upate kujifunza na kujua zaidi mambo mbalimbali kuhusu simu,mtandao,computer n.k . Pia usisahau kuandika comment zako hapo chini kwani ni za muhim sana.