Saturday, April 17, 2021

Jinsi ya kupata IMEI ( International Mobile Equipment Identity) ya simu yako

Neno IMEI ni kifupi cha International Mobile Equipment Identity. IMEI Ni number ambayo inatumiwa kukitambua na kutofautisha vifaa ambavyo vinatumia cellular network na huwa zipo tarakimu 15 katima IMEI . Cellular network ni network ambayo unatumia kupiga simu au kuunganishwa na internet. Kama simu yako ina sim card (laini) mbili,basi na IMEI zitakuwa mbili.

Umuhimu wa IMEI kwenye simu yako

1.Husaidia kuzuia wizi wa mobile devices.

2.kutambua na kutofautisha mobile devices pale inapoconnect kwenye mnara

Jinsi ya kupata au kujua IMEI ya simu yako.

1.kama simu yako ni ya kutoa betri ,IMEI waweza ipata kwa kuangalia nyuma ya simu yako baada ya kutoa betri la simu yako.

2.kama simu yako hairusu kutoa betri , utaweza kujua IMEI ya simu yako kwa kupiga code zifuatazo * # 06 #.

3. Kwa kwenda kwenye setting ya simu yako

Hatua ya kwanza. Nenda kwenye setting ya simu yako.

Hatua ya pili. Baada ya kubonyeza na kuingia kwenye setting za simu yako , chagua sehemu walipoandika about device

Hatua ya tatu. Baada ya kubonyeza sehemu ya abot devive hatua inayofata bonyeza status.

Hatua ya nne.Baada ya kubonyeza sehem iliyoandikwa status kinachofata ni kuona IMEI namba ya simu yako

NB; Ukifanya update zozote zile kwenye simu yako au ukibadilirisha sim card zako, IMEI number haibadiliki kwasababu imetengenezwa kama sehemu ya hardware ya simu. Wapo watu wanao badilisha IMEI namba na inawezekana lakini ni kosa kisheria kwa baadhi ya nchi.

No comments:

Post a Comment